SALA MBALIMBALI
Baba Yetu
Baba yetu uliye mbinguni
Jina lako litukuzwe
Ufalme wako ufike
Utakalo lifanyike
Duniani kama mbinguni
Utupe leo mkate wetu wa kila siku
Utusamehe makosa yetu
Kama tunavyowasamehe
Na sisi waliotukosea
Usitutie katika kishawishi
Lakini utuopoe maovuni.
Amina
Salamu Maria
Salamu Maria
Umejaa neema
Bwana yu nawe
Umebarikiwa kuliko wanawake wote
Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa
Maria Mtakatifu
Mama wa Mungu
Utuombee sisi wakosefu
Sasa, na saa ya kufa kwetu.
Amina.
Sala ya Asubuhi
Umenilinda usiku huu,
Ninakushukuru kwa moyo,
Ee Baba, Mwana na Roho,
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi nikutii,
Naomba sana Baba wee,
Baraka yako nipokee,
Bikira safi ee Maria,
Nisipotee unisimamie,
Mlinzi Mkuu Malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee,
Nitake nitende mema tu,
Na mwisho nije kwake juu.
Amina.
Nia Njema
Kumheshimu Mungu wangu
Namtolea roho yangu,
Nifanye kazi nipumzike
Amri zake tu nishike
Wazo, neno, tendo lote
Namtolea Mungu pote
Roho, mwili chote changu,
Pendo na uzima wangu
Mungu wangu nitampenda,
Wala dhambi sitatenda.
Jina lako nasifia,
Utakalo hutimia.
Kwa utii navumilia
Teso na matata pia.
Nipe, Bwana, neema zako
Niongeze sifa yako.
Amina.
Atukuzwe Baba
Atukuzwe Baba
na Mwana
na Roho Mtakatifu
Kama mwanzo
na sasa,
na siku zote,
na milele.
Amina
Atukuzwe Baba
na Mwana
na Roho Mtakatifu
Kama mwanzo
na sasa,
na siku zote,
na milele.
Amina
Kanuni ya Imani
Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu; aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu,
akazaliwa na Bikira Maria,
akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,
akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu;
siku ya tatu akafufuka katika wafu;
akapaa mbinguni; amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi;
toka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,
Kanisa takatifu katoliki,
ushirika wa Watakatifu,
maondoleo ya dhambi,
ufufuko wa miili, uzima wa milele.
Amina.
Sala ya Matumaini
Mungu wangu, natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu, neema zako duniani na utukufu mbinguni, kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi, nawe mwamini.
Amina.
Sala ya Imani
Mungu wangu, nasadiki maneno yote linalosadiki na linalofundisha kanisa katoliki la Roma; Kwani ndiwe uliyefundisha hayo, wala hudanganyiki, wala hudanganyi.
Sala ya Kutubu
Mungu wangu, nimetubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi. Basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema zako nipata kurudi.
LITANIA YA BIKIRA MARIA
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie. Bwana utuhurumie.
Kristo utuhurumie.
Kristo utuhurumie.
Bwana utuhurumie. Bwana utuhurumie.
Kristo utusikie. Kristo utusikilize
Baba wa mbinguni, Mungu, utuhurumie.
Mwana Mkombozi wa dunia, Mungu, utuhurumie.
Roho Mtakatifu, Mungu, utuhurumie.
Utatu Mtakatifu, Mungu mmoja, utuhurumie.
Kiitikio: Utuombee
Maria Mtakatifu,
Mzazi Mtakatifu wa Mungu,
Bikira Mtakatifu, Mkuu wa mabikira,
Mama wa Kristu,
Mama wa neema ya Mungu,
Mama mtakatifu sana,
Mama mwenye usafi wa moyo,
Mama usiye na doa,
Mama usiye na dhambi,
Mama mpendelevu,
Mama mstaajabivu,
Mama wa shauri jema,
Mama wa Mwumba,
Mama wa Mkombozi,
Bikira mwenye utaratibu,
Bikira mwenye heshima,
Bikira mwenye sifa,
Bikira mwenye enzi,
Bikira mwenye huruma,
Bikira amini,
Kikao cha haki,
Kikao cha hekima,
Sababu ya furaha yetu,
Chombo cha neema,
Chombo cha heshima,
Chombo bora cha ibada,
Waridi lenye fumbo,
Mnara wa Daudi,
Mnara wa pembe,
Nyumba ya dhahabu,
Sanduku la Agano,
Mlango wa mbingu,
Nyota ya asubuhi,
Afya ya wagonjwa,
Makimbilio ya wakosefu,
Mfariji wa wenye uchungu,
Msaada wa Wakristu,
Malkia wa Malaika,
Malkia wa Mababu,
Malkia wa Manabii,
Malkia wa Mitume,
Malkia wa Mashaidi,
Malkia wa Waungama,
Malkia wa Mabikira,
Malkia wa Watakatifu wote,
Malkia uliyeumbwa, pasipo dhambi ya asili,
Malkia uliyepalizwa mbinguni,
Malkia wa Rozari takatifu,
Malkia wa amani.
****
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusamehe, Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utusikilize, Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia, utuhurumie.
K. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristu.
TUOMBE: Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na ya mwili sikuzote. Tuopolewe na mashaka ya sasa kwa maombezi ya Maria mtakatifu, Bikira daima, ili tupate na furaha ya milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina
Sala ya Mapendo
Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza.
Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako..
Amina.
Sala ya usiku
Sasa siku imekwisha,
Kwako Mungu napandisha,
moyo wangu kwa shukrani,
nipumzike kwa amani,
Mema mengi umenipa,
ninashindwa kukulipa,
Baba mwema ondolea,
yote niliyokosea.
Yesu mpenzi unijie,
ombi langu usikie,
unifiche mtoto wako,
ndani ya jeraha zako,
Ewe Mama unipe neema,
raha na usiku mwema,
Roho mlizi ukakeshe,
pepo wasinikoseshe
Naiweka roho yangu,
mikononi mwa Baba yangu,
bila hofu napumzika,
mwisho kwake nitafika.
MATENDO YA FURAHA
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
1.Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu.
Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
Amina.
MATENDO YA MWANGA (ALHAMISI)
1. Yesu anabatizwa Mto Jordani.
Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
2. Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana.
Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya Injili.
3. Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu.
Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
4. Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
5. Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristi.
Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
1. Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
2. Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
3. Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
4. Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
5. Yesu anakufa Msalabani.
Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
Amina.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumapili na Jumatano)
1.Yesu anafufuka.
Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
2. Yesu anapaa mbinguni.
Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
3. Roho Mtakatifu anawashukia Mitume.
Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
4. Bikira Maria anapalizwa mbinguni.
Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
5. Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni.
Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema
Amina.
Sala ya Imani
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote.
Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza.
Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako.
Amina
Amri za Mungu
1. Ndimi Bwana Mungu wako usiabudu miungu mingine.
2. Usilitaje bure jina la Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini,
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
Amri za Kanisa
1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya Jumatano ya majivu, usile nyama siku ya Ijumaa kuu.
3. Ungama dhambi zako zote walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka.
5. Saidia Kanisa Katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria Katoliki za ndoa.
Malaika wa Bwana
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Salamu, Maria,.....
Ndimi mtumishi wa Bwana.
Nitendewe ulivyonena.
Salamu, Maria....
Neno la Mungu akatwaa mwili.
Akakaa kwetu.
Salamu, Maria....
Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu.
Tujaliwe ahadi za Kristu.
Tuombe
Tunakuomba, Ee Bwana, utie neema yako mioyon mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu kwa mateso na msalaba wake tufikishwe kwenye utukufu na ufufuko.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
Amina
Tunakimbilia
Tunakimbilia, Ulinzi wako mzazi Mtakatifu wa Mungu, Usitunyime tukiomba katika shida zetu, Utuokoe siku zote kila tuingiapo hatarini, Ee Bikira Mtukufu na mwenye Baraka.
Amina
Sala ya Mtakatifu Inyasi
Roho ya Kristu, nitakase
Mwili wa Kristu, niokoe
Damu ya Kristu, nifurahishe
Maji ya ubavu wake Kristu, nioshe
Mateso ya Kristu, nguvu nizidishie
Ee Yesu mwema unisikilize
Katika madonda yako unifiche
Usikubali nitengwe nawe
Na adui mwovu, unikinge
Saa ya kufa kwangu, unite
Uniamuru nikusogelee
Sifa zako niimbe
Na watakatifu wako,
milele, milele
Amina
Kanuni ya Imani ya NICEA
Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi
Mwumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristu,mwana wa pekee wa Mungu.
Aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote.
Mungu aliyetoka kwa Mungu,mwanga kwa mwanga,Mungu kweli kwa Mungu kweli.
Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba,
ambaye vitu vyote vimeumbwa naye.
Ameshuka toka mbinguni kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu.
Akapata mwili kwa uwezo wa roho mtakatifu kwake yeye Bikira Maria akawa mwanadamu.
Akasulibiwa pia kwa ajili yetu sisi
Akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,akafa akazikwa.
Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa.
Akapaa mbiguni, amekaa kuume kwa baba
Atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu nao ufalme wake hautakuwa na mwisho
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu Bwana mleta uzima atokaye kwa Baba na Mwana anayeabudiwa na kutukuzwa
pamoja na Baba na Mwana aliyenena kwa vinywa vya manabii.
Nasadiki kwa Kanisa moja,Takatifu Katoliki la mitume
Naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu.
Na uzima wa milele ijayo.
Amina.
Sala ya Majitoleo
Ee Yesu, kupitia mikono safi ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, kazi, masumbuko, na furaha zangu zote za siku hii ya leo, kwa ajili ya nia za Moyo wako Mtakatifu, Ee Yesu ufalme wako utufikie!
Amina
🙏🙏🙏🙏🙏💞🌺🪴💐💕💓💖💐
ReplyDelete