Posts

Showing posts from December, 2022

SALA YA JIONI.

 + TUSALI SALA YA JONI Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina. Tunakushukuru ee Mungu kwa mema yote uliyotujalia sikuu hii ya leo. BABA YETU. Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina. SALAMU MARIA. Salam Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. SALA YA IMANI. Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina. SALA YA MATUMAINI. Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe...

SALA YA ASUBUHI

  TUSALI SALA YA ASUBUHI. + Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Ee Baba yetu Mungu mkuu, Umenilinda usiku huu. Nakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho. Nilinde tena siku hii, Niache dhambi, nikutii. Naomba sana Baba wee, Baraka zako nipokee. Bikira safi, Ee Maria Nisipotee nisimamie. Mlinzi mkuu malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwako juu. Amina. • NIA NJEMA. Kumheshimu Mungu wangu Namtolea roho yangu, Nifanye kazi nipumzike Amri zake tu nishike Wazo, neno, tendo lote Namtolea Mungu pote Roho, mwili chote changu, Pendo na uzima wangu Mungu wangu nitampenda, Wala dhambi sitatenda. Jina lako nasifia, Utakalo hutimia. Kwa utii navumilia Teso na matata pia. Nipe, Bwana, neema zako Niongeze sifa yako. Amina. •SALA YA MATOLEO Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie. • BABA YETU. Baba yetu uliye ...

MALIKIA WA MBINGU

 + MALIKIA WA MBINGU Malkia wa mbingu furahi, Aleluya! Kiitikio: Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya! Amefufuka kama alivyosema, Aleluya! Kiitikio: Utuombee kwa Mungu, Aleluya! Furahi, shangilia ee Bikira Maria, Aleluya! Kiitikio: Kwani hakika Bwana amefufuka, Aleluya!

SALA YA KUTUBU

+  SALA YA KUTUBU. Mungu wangu, nimetubu sana dhambi zangu. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako, nipate kurudi. Amina.

SALA YA MALAIKA MLINZI

  + SALA KWA MALAIKA MLINZI. Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote, za roho na za mwili. Amina.

SALA YA MAPENDO

• SALA YA MAPENDO. Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.

SALA YA MATUMAINI

  • SALA YA IMANI. Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.

AMRI ZA KANISA.

  • AMRI ZA KANISA 1. Hudhuria misa takatifu, dominika na sikukuu zilizoamriwa. 2. Funga siku ya jumatano ya majivu; usile nyama siku ya ijumaa kuu. 3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka. 4. Pokea Ekaristi takatifu hasa wakati wa Paska. 5. Saidia kanisa katoliki kwa zaka. 6. Shika sheria katoliki za ndoa.

AMRI ZA MUNGU

  • AMRI ZA MUNGU. 1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu Miungu wengine. 2. Usilitaje bure jina la Mungu wako. 3. Shika kitakatifu siku ya Mungu. 4. Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na heri duniani. 5. Usiue. 6. Usizini. 7. Usiibe. 8. Usiseme uongo. 9. Usitamani mwanamke asiye mke wako. 10. Usitamani mali ya mtu mwingine.

SALA YA JIONI

TUSALI SALA YA ASUBUHI. + Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Ee Baba yetu Mungu mkuu, Umenilinda usiku huu. Nakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho. Nilinde tena siku hii, Niache dhambi, nikutii. Naomba sana Baba wee, Baraka zako nipokee. Bikira safi, Ee Maria Nisipotee nisimamie. Mlinzi mkuu malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwako juu. Amina. • NIA NJEMA. Kumheshimu Mungu wangu Namtolea roho yangu, Nifanye kazi nipumzike Amri zake tu nishike Wazo, neno, tendo lote Namtolea Mungu pote Roho, mwili chote changu, Pendo na uzima wangu Mungu wangu nitampenda, Wala dhambi sitatenda. Jina lako nasifia, Utakalo hutimia. Kwa utii navumilia Teso na matata pia. Nipe, Bwana, neema zako Niongeze sifa yako. Amina. •SALA YA MATOLEO Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie. • BABA YETU. Baba yetu uliye mbingu...