+ TUSALI SALA YA JONI Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina. Tunakushukuru ee Mungu kwa mema yote uliyotujalia sikuu hii ya leo. BABA YETU. Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina. SALAMU MARIA. Salam Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. SALA YA IMANI. Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina. SALA YA MATUMAINI. Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe...
TUSALI SALA YA ASUBUHI. + Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Ee Baba yetu Mungu mkuu, Umenilinda usiku huu. Nakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho. Nilinde tena siku hii, Niache dhambi, nikutii. Naomba sana Baba wee, Baraka zako nipokee. Bikira safi, Ee Maria Nisipotee nisimamie. Mlinzi mkuu malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwako juu. Amina. • NIA NJEMA. Kumheshimu Mungu wangu Namtolea roho yangu, Nifanye kazi nipumzike Amri zake tu nishike Wazo, neno, tendo lote Namtolea Mungu pote Roho, mwili chote changu, Pendo na uzima wangu Mungu wangu nitampenda, Wala dhambi sitatenda. Jina lako nasifia, Utakalo hutimia. Kwa utii navumilia Teso na matata pia. Nipe, Bwana, neema zako Niongeze sifa yako. Amina. •SALA YA MATOLEO Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie. • BABA YETU. Baba yetu uliye ...
Comments
Post a Comment